Saturday, 7 November 2015

WASYRIA WATAKIWA KUFANYA MAZUNGUMZO

Vyama vya siasa nchini Syria vimesema kutumia njia za kisiasa na mazungumzo baina ya Wasyria wenyewe ndilo chaguo pekee la kumaliza mgogoro wa nchi hiyo. Vyama hivyo vimetoa sisitizo hilo katika kikao maalumu kilichofanyika jana Jumamosi mjini Damascus chini ya anuani: "Utatuzi wa kisiasa wa mgogoro wa Syria" na kueleza kwamba kuna ulazima wa kufanyika mazungumzo baina ya Wasyria wenyewe kwa kushirikisha vyama na makundi yote ya nchi hiyo.Washiriki wa kikao hicho kilichohudhuriwa pia na Waziri wa Maridhiano ya Kitaifa ya Syria Ali Haidar, wawakilishi wa vyama vya siasa na wa asasi za kiraia za nchi hiyo wametangaza kuwa kuna ulazima wa kushirikishwa taasisi zote za kisiasa na kijamii kwa ajili ya kupanga hatima ya baadaye ya nchi hiyo na kupambana na ugaidi na fikra za kitakfiri.
Waziri wa Maridhiano ya Kitaifa ya Syria amesisitiza kuwa njia yoyote ya ufumbuzi wa mgogoro wa nchi hiyo lazima idhamini maisha ya salama na kuishi kwa masikilizano watu wa makabila, dini na madhehebu zote nchini humo.

No comments:

Post a Comment