Saturday, 7 November 2015

JESHI LA YEMEN LAHARIBU MELI YA KIVITA YA SAUDIA


Jeshi la Yemen limetangaza kuwa limelipua meli nyingine ya kivita ya unaoitwa muungano wa nchi za Kiarabu unaoongozwa na Saudi Arabia katika mashambulizi dhidi ya Waislamu wa Yemen.
Taarifa iliyotolewa na jeshi la Yemen imesema, jeshi hilo limefanikiwa kushambulia na kuzamisha majini meli ya nne ya kivita ya Saudi Arabia baada ya kuilenga kwa maroketi katika pwani ya al Makha huko kusini magharibi mwa Yemen. Mapema jana pia makundi ya wapiganaji wa kujitolea yalitangaza kuwa yamezamisha boti ya wavamizi wa Kisaudi kusini mwa nchi hiyo.
Katika upande mwingine ndege za kivita za Saudi Arabia zimeendelea kufanya mashambulizi katika maeneo mbalimbali ya Yemen ambayo yameua idadi kadhaa ya raia wasio na hatia. Vilevile kumeripotiwa mapigano makali kati ya jeshi la Yemen na vibaraka wa Saudia katika mkoa wa Aden ambapo mamluki kadhaa wameangamizwa.
Saudi Arabia na waitifaki wake tarehe 26 Machi mwaka huu walianzisha mashambulizi dhidi ya wananchi wa Yemen kwa kisingizio cha kuirejesha madarakani serikali iliyojiuzulu. Maelfu ya raia wameuawa na wengine wengi kulazimika kuwa wakimbizi kutokana na mashambulizi hayo.

No comments:

Post a Comment